Frashvortex

Friday

TANZANIA IMEELEZA MSIMAMO WAKE KUHUSU MGOGORO WA MPAKA KATIKA ZIWA NYASA


Tanzania imeeleza msimamo wake kuhusu mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa baina yake na nchi ya Malawi na kubainisha kuwa bado inayoimani na Jopo la usuluhishi linaloongozwa na Rais wa Mozambiq JOACHIM CHISANO.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa BENARD MEMBE amesema wanashangazwa na hatua ya Rais wa Malawi Bi. JOYCE BANDA kutangaza kuupeleka mgogoro huo mahakamani kabla ya Jopo la Usuluhishi kukamilisha kazi yake wakati akijua kufanya hivyo ni kukiuka makubaliano waliyoingia Novemba 2012.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri MEMBE ameitaka nchi ya Malawi kusubiri uamuzi wa Jopo la Usuluhishi na kutoigusa sehemu ya mpaka iliyopo katikati ya Ziwa Nyasa mpaka hapo mgogoro uliopo utakapopatiwa ufumbuzi.
Katika hatua nyingine Waziri MEMBE amesema tayari Serikali imekubali kupeleka wanajeshi 850 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo inasubiri ridhaa ya Bunge ili kutekeleza uamuzi huo unaotokana na makubaliano ya nchi za SADC

No comments:

Post a Comment