Waziri Mkuu wa Tanzania MIZENGO PINDA leo
amezindua rasmi ripoti ya idadi ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 katika
ngazi za Mikoa,Wilaya,Kata na Shehia, ambapo katika ripoti hiyo takwimu
zinaonyesha kuwa Mkoa wa DAR ES SALAAM umeongoza kwa kuwa na watu
Milioni 4.3 likiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 5.5.
Aidha
katika ripoti hiyo Mkoa wa MWANZA umeshika nafasi ya pili kwa kuwa na
jumla ya Watu Milioni 2.7, sawa na ongezeko la asilimia 4 .3
kulinganisha na takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002, huku
mkoa wa mpya wa KATAVI ukitajwa kuwa ndio mkoa wenye idadi ndogo zaidi
ya watu kwa kuwa na watu laki Tano na Elfu Sitini pekee.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo Waziri Mkuu PINDA, amewataka
watendaji wote wa Serikali katika ngazi za Mkoa na Wilaya kuhakikisha
wanaongeza jitihada za utendaji wao.Katika hatua nyingine PINDA ametoa
rai kwa Watanzania kuzingatia mfumo wa uzazi kwa Mpango ili kuipunguzia
serikali mzigo.
Kwa upande wake
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa
Sensa ya Watu na Mkazi mwaka 2012, BALOZI SEIF ALLY IDDI amesema matokeo
hayo yameibua changamoto nyingi.Matokeo ya jumla ya sensa ya watu na
Makazi kwa mwaka 2012 yalizinduliwa rasmi Desemba 31 mwaka jana na Rais
wa Tanzania Dokta JAKAYA KIKWETE na kuonyesha kuwa idadi ya watu
TANZANIA imeongezeka na kufikia Milioni 44.9.
Sensa
ya kwanza Tanzania ilifanyika mwaka 1910,huku Sensa nne za Mwisho
zikifanyika baada ya Uhuru katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na
2002,ambapo Kulingana na sensa ya mwisho iliyofanyika mwezi Agosti mwaka
2002, idadi ya watu Tanzania ilikuwa Milioni 34,4
No comments:
Post a Comment